Kesi za ukatili wa polisi ziliongezeka maradufu katika mwaka jana – IMLU

0

Wanachama wa shirika la Matibabu na Kisheria (IMLU) wakati wa mkutano na wanahabari jijini Nairobi Alhamisi 14.

Septemba 14, 2023 Takriban kesi 128 za mauaji ya kiholela zimerekodiwa nchini Kenya katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.

Katika ripoti iliyotolewa na shirika huru la kimatibabu na sheria (IMLU) Alhamisi, ilifichua kuwa kesi hizo zilirekodiwa kati ya Okt 2022 na Agosti 2023.

Ripoti hizo zinasema kuwa kesi zinazohusiana na utesaji na ukiukaji wa haki za binadamu ziliongezeka maradufu katika muda huo ikilinganishwa na miaka iliyopita, kutoka 232 hadi 482.

Kesi hizo ni pamoja na mateso, kunyongwa na ukiukaji wa haki za binadamu.

“Hii inaashiria ongezeko kubwa la kesi 250 ikilinganishwa na ukiukwaji 232 ulioripotiwa katika kipindi kama hicho cha 2021-2022,” taarifa hio ilionyesha. .

Kati ya kesi 482,  351 zilikuwa za mateso, unyama, udhalilishaji au adhabu, IMLU inafichua. Kwa kuangalia jinsia na umri, ilibainika kuwa wengi wa wahathiriwa/wanusurika walikuwa vijana wa kiume wenye umri wa miaka 18-35, ambao ni 314.

Wale wenye umri wa miaka 36-65 walikuwa 121, miaka 0-17 walikuwa 44, na wale walio zaidi ya miaka 36-65. 65 ilijumuisha watu 3. Kwa jumla kati ya kesi 482, 415 walikuwa wanaume na 67 wanawake.

IMLU iliongeza kwamba ongezeko kubwa la visa vya mateso na ukiukaji linaonyesha kushindwa kudhibiti utumizi mbaya wa mamlaka ya polisi ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya bunduki.

“Ongezeko hili la kutisha halionyeshi tu ukosefu wa maendeleo bali pia linaonyesha kuwa hali imekuwa mbaya zaidi,” ilisema taarifa hiyo.

Baada ya kushika wadhifa huo kama rais wa tano wa Kenya, Rais Ruto aliamuru uchunguzi ufanywe kuhusu mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutokea katika utawala uliopita.

Hii ilishuhudia baadhi ya wapelelezi wakihangaika kuhusu kutoweka na mauaji ya watu. Haya yanajiri baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani kusema mauaji ya kiholela yaliotokea nchini yanachunguzwa kikamilifu.

Ripoti na James Mutua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *