MultiChoice Kenya Yazindua Mpango Mpya wa Upeperushaji wa Gotv kwa Wateja Wake

0

Nairobi, Disemba 1, 2023: MultiChoice Kenya, kampuni inayoongoza barani Afrika kwa kutoa burudani, Ijumaa Mosi ilizindua mpango mpya wa upeperushaji wa GOtv Stream, kukaribisha msimu wa sikukuu huku ikihaidi bei za urahisi kwa wateja wake ili kufuatilia vipindi, sinema, na michezo kwenye simu za mkononi, kompyuta, na mitandaoni.

Programu ya GOtv Stream ni huduma iliyoundwa kuwaburudisha wateja wakati wowote na mahali popote. Kupitia programu hii, wateja wanaweza kutazama televisheni moja kwa moja na kufurahia GOtv Catch Up na kufikia kufaidika na huduma nyingi.

Programu hii itawawezesha wateja kuanzisha akaunti ya kibinafsi kulingana na kifurushi ambacho wamelipia. Baadhi ya vifurushi vya GOtv ni Supa Plus, Supa, Max, Plus, na Lite.

Ili kupata huduma hii, wateja watahitaji kuwa na usajili wa GOtv, kifaa kinachoweza kutumika, Kitambulisho cha MultiChoice, na muunganisho wa intaneti. Ingawa yeyote anaweza kutumia mfumo wa GOtv Stream, ni wateja wa GOtv pekee wanaoweza kufurahia vituo vya televisheni kulingana na vifurushi walivyolipia.

App ya GOtv Stream itapatikana kwenye vifaa vinavyotumia Android na IOS na watumiaji watapewa ruhusa kuandikisha hadi vifaa vinne kwenye akaunti yao ya GOtv Stream lakini upeperushaji utakuwa kwa kifaa kimoja kwa wakati mmoja.

Kulingana na Nzola Miranda, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Kenya:

Hii ni hatua muhimu katika jitihada zetu za kuendelea kutumia teknolojia na uvumbuzi ili kuridhisha wateja wetu na kuhakikisha kuwa wanapata burudani ya kutosha.

Nzola Miranda

Kwa upande wake, Elisha Kamau, Meneja wa mahusiano MultiChoice Kenya, alisema,

Tunafurahi kuzindua app ya upeperushaji ya GOtv Stream kwa wateja wetu. App hii inaambatana na ahadi yetu ya kutoa burudani ya hali ya juu inayokidhi mahitaji na mapendeleo ya wateja wetu

Elisha Kamau

Programu hio mpya itawawezesha wateja kupakua hadi video 25 kwa wakati mmoja. Video zilizopakuliwa zitadumu kwa siku 30. Mara tu inapotazamwa, video iliyopakuliwa hudumu masaa 48. Programu hio pia itawezesha wateja kubinafsisha vizuizi kwa watoto ili kuhakikisha usalama wao.

Ripoti na James Mutua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *